Jana jumapili tarehe 19 Desemba 2010 nilipata bahati ya kuwa miongoni mwa waumini wa Kanisa la Anglikana ambao walihudhuria uzinduzi wa kanisa jipya la Mtakatifu Francis wa Xsavia pale wilayani Mkuranga.
Kikubwa nilichojifunza ni moyo wa kujitolea waliounyesha waumini wa Kanisa hilo katika kufanikisha suala hili la kimaendeleo, pamoja na uchache wao lakini waliweza kufikia lengo.Pia moyo wa ujasili na uzalendo wa Mtumishi wa Mungu kiongozi wa kigango hicho ambaye kimsingi anastahili sifa za kipekee kwa kufanikisha kazi hii kubwa. Bwana awabariki wote walioshiriki katika kufanikisha jambo hilo.AMEN
No comments:
Post a Comment